NAFASI NA MCHANGO WAKO KATIKA KANISA
1 Kor 12:28
"Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa ,wa kwanza mitume,wa pili manabii,wa tatu waalimu,kisha miujiza,kisha karama za kuponya wagonjwa,kisha masaidiano,na maongozi,na aina za lugha"
Je,unafahamu karama ulizonazo?
Je unafahamu Mungu amekuweka kwenye Huduma gani sasa?
kama unafahamu je unazitumiaje na huduma ulimo katika kuujenga Mwili wa Kristo?
Tunaalikwa kumwomba Mungu atuwezeshe kutumia vema Karama alizotupa ndani ya Huduma mbalimbali katika Kanisa.
Mungu atubariki sote maana kwa Pamoja tutaitika wito na kumwambia Mungu "tuko tayari kufanya kazi yako".Kama uko tayari kufanya kazi ya Mungu tusali pamoja sala hii:
SALA
"Ee Mungu Mkuu tunaomba kwa Huruma yako tuwezeshe kuitoa miili yetu iwe dhabihu hai mbele zako ili tuweze kufanya kweli kazi yako sawasawa na makusudi yako kwetu.Dhihirisha karama ulizotupa ndani yetu Mungu,tujaze na karama zote uzionazo tunazihitaji,tuwezeshe kuzifahamu na utuunganishe katika Huduma ulizotuwekea tufanye kazi yako kwa Sifa yako,Heshima na Utukufu wako nyakati zote.Kwa Jina la Yesu tunaomba na kushukuru na kuamini,AMINA.
No comments:
Post a Comment