Monday, January 28, 2013

SEMINA YA ROHO MTAKATIFU

Semina ya Roho Mtakatifu imeanza jumapili tarehe 27/01/2013 katika mkutano wa sala wa vijana Nyajahoja saa sita mpaka nane mchana.

Yaliyofundishwa:
1.Roho Mtakatifu ni nani
2.Kubatizwa katika Roho Mtakatifu
3.Aina za Roho
4.Kazi za Roho Mtakatifu.

Semina hii itaendelea tena jumapili ijayo tarehe 03/02/2013.
Karibuni wote tuendelee kupata mafundisho yatakayotujenga na kutuimarisha kiroho.

Sunday, January 27, 2013

KUMALIZA MWAKA

Tunamshukuru Mungu tumeweza kumaliza mwaka kwa kuwa na mikesha miwili.Mikesha hiyo ilifanyika Retreat centre SAUT tarehe 8/12/2012 na tarehe 15/12/2012.Masomo yaliyofundishwa yatakuwa yanapatikana katika blog hii mapema iwezekanavyo.Tunawashukuru wote walioweza kuhudhuria na kushiriki,MUNGU ATUBARIKI SOTE.

Wednesday, December 5, 2012

SIKU YA KUSHUKURU

Tunamshukuru Mungu tuliweza kuandaa na kufanya siku ya kumshukuru Mungu vijana.siku hiyo ilikuwa tarehe 4/11/2012 na ilifanyika chuo cha Butimba.
Shukrani ziwafikie wote waliofanikisha shughuli hiyo.
Mungu atubariki sote

Tuesday, September 25, 2012

UJUMBE MKUTANO WA SALA VIJANA 23/09/2012

NAFASI NA MCHANGO WAKO KATIKA KANISA
1 Kor 12:28
"Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa ,wa kwanza mitume,wa pili manabii,wa tatu waalimu,kisha miujiza,kisha karama za kuponya wagonjwa,kisha masaidiano,na maongozi,na aina za lugha"

Je,unafahamu karama ulizonazo?
Je unafahamu Mungu amekuweka kwenye Huduma gani sasa?
kama unafahamu je unazitumiaje na huduma ulimo katika kuujenga Mwili wa Kristo?

Tunaalikwa kumwomba Mungu atuwezeshe kutumia vema Karama alizotupa ndani ya Huduma mbalimbali katika Kanisa.

Mungu atubariki sote maana kwa Pamoja tutaitika wito na kumwambia Mungu "tuko tayari kufanya kazi yako".Kama uko tayari kufanya kazi ya Mungu tusali pamoja sala hii:

SALA
"Ee Mungu Mkuu tunaomba kwa Huruma yako tuwezeshe kuitoa miili yetu iwe dhabihu hai mbele zako ili tuweze kufanya kweli kazi yako sawasawa na makusudi yako kwetu.Dhihirisha karama ulizotupa ndani yetu  Mungu,tujaze na karama zote uzionazo tunazihitaji,tuwezeshe kuzifahamu na utuunganishe katika Huduma ulizotuwekea tufanye kazi yako kwa Sifa yako,Heshima na Utukufu wako nyakati zote.Kwa Jina la Yesu tunaomba na kushukuru na kuamini,AMINA.

Monday, September 17, 2012

BAADHI YA MAMBO MUHIMU YA KUOMBEA MWEZI HUU

1. Rum 12:1-2
i)Mungu kwa huruma yake atupatie neema/atuwezeshe kuitoa miili yetu iwe dhabihu iliyo hai kwake Mungu.
ii)Tufanywe upya nia zetu
iii)Thue mapenzi ya Mungu katika mambo yote

2.Efe 6:10-18
i)Utayari wa kufanya kazi ya Mungu wakati wote -ufaao na usiofaa
ii)Utayari wa kuomba msaada wa Roho Mtakatifu kila wakati na kutembea nae katika yote.
iii)Tuweze kutumia vema karama tulizopewa katika huduma tunazopewa kwa sifa na utukufu wa jina lake

3.Watendakazi katika shamba la Bwana

4.Nidhamu katika maombi Efe 6:10-19

5.Yoh 17 Mungu atupe umoja,ulinzi na utukufu wake Mungu viwe pamoja nasi

6.Siku ya kushukuru itakayofanyika mwezi wa 10